Kikombe Changu Kinafurika
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 23:5,6 Waandaa meza mbele yangu, machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, na kikombe changu kinafurika. Hakika wema na fadhili zitanifuata siku zote za maisha yangu; nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.
Kuna watu ambao kwa asili ni wakosoaji, Kawaida wana tabia ya kuona mambo yote ni mabaya huku wakichunguza kila kitu. Wengine kwa asili ni wenye msimamo wa kutegemea mazuri. wanapanga mambo kwa ujasiri lakini bado kuna aina nyingine ya watu.
Mtu mmoja anaweza kuona kama kikombe kimejaa maji na mwingine akaona kama kiko nusu, Mimi ni mtu anayeona kwamba kikombe kiko nusu. Ninaona bado kuna uwezekano wa kutimiza jambo fulani hata kama mazingira hayaridhishi, Lakini, ili nipate uwiano sasa, nina watu wa karibu wenye mtazamo wa kuona kama kikombe kiko nusu, ili nisipelekwe na maoni yangu tu.
Lakini hawa wengine wa aina ya tatu ni akina gani? Hawa hawafanani na makundi mawili ya kwanza. Mimi ninawaita watu wenye “vikombe vinavyofurika.”
Zaburi 23:5,6 Waandaa meza mbele yangu, machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, na kikombe changu kinafurika. Hakika wema na fadhili zitanifuata siku zote za maisha yangu; nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.
Hapo tuna Zaburi nyingine ya Daudi, mtu aliyekuwa na adui wengi mno. Lakini alijifunza kwamba hata akiwa katika hatari ya namna gani, Mungu bado alikuwa naye mahali pale. Angalia anavyochora picha ya ajabu-ajabu:
Waandaa meza mbele yangu, machoni pa watesi wangu.
Adui wanashambulia wakipanda na kuenea mlima mzima lakini Mungu ameandaa meza, yaani karama mbele yake. Daudi haoni kikombe kama kiko nusu ama kimejaa, Kikombe chake kinafurika. Kwanini? Ni kwasababu anajua kwamba Mungu yuko naye mahali pale pale.
Hakika wema na fadhili zitanifuata siku zote za maisha yangu; nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.