Kilele cha Siwa Barafu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yakobo 5:10,11 Ndugu, watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu. Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.
Mafanikio ni neno ambalo sisi sote tungependa kulikumbatia. Je! Kuna mtu asiyetaka kufaulu na kufanikisha jambo ambalo amekusudia kulifanya? Lakini hata kama mafanikio yanavishawishi vyake, bado ni dhana yenye udanganyifu.
Usinielewe vibaya, sisemi mafanikio ni mabaya, lakini kwa upande mmoja, mtu anaweza kujitahidi kupata mafanikio katika mambo yasiyofaa, au kwa makusudi potovu au kwa njia isiyo halali. Hii ndio ilikuwa tabia yangu zamani kwa sehemu ya kwanza ya maisha yangu na nisingeweza kumshauri mtu aifuate hata kidogo.
Lakini kwa upande wa pili, ni jambo jema kujitoa na kumtumikia Bwana kwa nguvu zote; kutii wito wake, na kujitahidi kabisa chini ya mkono wake na kwa nguvu zake ili tutimize mpango wake kwa ajili ya utukufu wake.
Watwaeni manabii wa Agano la Kale wawe mfano, akina Isaya, Ezekieli, Ayubu na wengine – ni rahisi mtu kufikiri kwamba walifanikiwa katika huduma yao. Lakini subiri kwanza, tuangalie vizuri kama hiyo ni kweli.
Yakobo 5:10,11 Ndugu, watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu. Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.
Ina maana, “mafanikio” yetu; wengine wanaoona kama ni kilele tu kama barafu inayoelea baharini. Sehemu yake kubwa inabaki chini ya maji na mtu anaona kilele tu. Na chini ya mafanikio yetu, watu hawaoni kazi ngumu tuliyoifanya, ustahimili, kukesha, kukataliwa, kujitolea, nidhamu, kukosolewa, mashaka, kufeli, na hatari – yaani hayo yote tuliyoyapitia ili tufanikishe lengo letu. Mafanikio katika Ufalme wa Mungu yanatakiwa yapitie hayo yote.
Lakini kumbuka, magumu hayo yote yanatudhihirishia kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.