... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kipindi cha Majaribu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mariko 1:12,13 Mara Roho akamtoa aende nyikani. Akawako huko jangwani siku arobaini, hali akijaribiwa na Shetani; naye alikuwa pamoja na wanyama wa mwitu, na malaika walikuwa wakimhudumia.

Listen to the radio broadcast of

Kipindi cha Majaribu


Download audio file

Mambo yanatubana vibaya – aidha kimwili, kihisia au kiroho – sijui kama umeshaona,  hapo ndipo majaribu yanakujia kasi.  Ni kama kuna mtu anayeona jinsi unavyopambana, ndio maana anafurahia kupata nafasi kukupiga teke wakati umeshaangushwa.

Majaribu ni mada tusiyopenda kuijadili sana.  Ni kwasababu tunaogopa mawazo ya watu wengine.  Kwanini?  Inawezekana tunaogopa kwasababu tumedanganyika kwa kufikiri kwamba ni sisi tu; tunaojaribiwa.

Lakini hii si kweli hata kidogo.  Majaribu yanatufikia sisi sote, hususani pale tunapobanwa na mambo; hususani wewe ni mtu anayetaka kumheshimu Mungu kwa moyo wote.  Hakuna anayepewa nafuu katika hilo.  Hata Yesu hakupewa.

Mariko 1:12,13  Mara Roho akamtoa aende nyikani.  Akawako huko jangwani siku arobaini, hali akijaribiwa na Shetani; naye alikuwa pamoja na wanyama wa mwitu, na malaika walikuwa wakimhudumia.

Mazingira ya Yesu yalitisha mno. Roho alikuwa amemtupa jangwani katikati ya wanyama pori, bila chakula, akakosa kula siku arobaini mchana na usiku.  Alikuwa dhaifu na kubanwa pande zote, halafu ndipo Shetani alimjia ili amjaribu.

Je!, Mazingira kama hayo, si umeshayaona?  Lakini; hata katika mazingira mabaya, Mungu alikuwa pamoja naye.  Palepale, katika mazingira yale magumu, Baba yake alikuwa pamoja naye hata kama yeye alijisikia mpweke.  Halafu kwa muda mwafaka, malaika walikuwa wakimhudumia.

Si wewe tu peke yako unayejaribiwa, wala hauko peke yako.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy