Kisha, Maisha Yanaendelea Tu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Luka 2:40 Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.
Hivi karibuni, swala zima la Krismas litakuwa limeshapita kwenye kalenda yetu na kutoweka. Na sisi tutaendelea na maisha kama kawaida. Lakini huko mbeleni, itakuaje?
Asilimia tisini na tisa ya maisha – maisha yako na ya kwangu – yanahusu “mambo ya kawaida”. Kwa wengi, ni mlolongo wa kazi, siku tano kwa wiki, wikendi ya siku mbili, kazi ngumu isioisha, pamoja na kupumzika kidogo kipindi tunachokiita “likizo”.
Mfumo huo unaweza kubadilika baada ya miaka kadhaa, lakini kwa kweli maisha ya kila mtu yanafuata mfumo huo huo tukitofautiana ni kidogo tu. Na ndivyo ilivyokuwa hata kwa kijana Yesu, yule ambaye tumetoka kusherehekea kuzaliwa kwake.
Ndiyo, yeye na wazazi wake ilibidi wakimbilie Misri kwa muda ili asiuawe na Herode. Lakini wakati walirejea Nazareti, mfumo wa maisha ya kila siku ulianza tena. Tumepewa kwa nadra sana habari za utoto wa Yesu. Mstari unaofuata ni katika mistari michache inayoeleza habari ya kipindi cha ujana wake:
Luka 2:40 Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.
Lakini maandiko haya machache yamejaa maana sana. Alikuwepo pale kwenye kituo cha useremala cha baba yake akijifunza ufundi ule halafu tunasoma nini? Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima.
Mwitikio wa Mungu ulikuwa upi? Neema ya Mungu ilikuwa juu yake.
Sote tunapitia vipindi visivyovutia katika maisha, tusionekane, tukijifunza fani fulani … lakini hata katika hatua zile za kawaida, hasa hapo ulipo, Mungu anao mpango kwa ajili yako kama alivyokuwa nao kwa ajili ya Mwanae.
Mpango wa kukuandaa, kufanya ukue, uwe mtu mzima, kukujaza hekima … na kukubariki. Mungu anao mpango.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.