... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kitu Mungu Anachokitaka

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Amosi 5:21-24 Mimi nazichukia sikukuu zenu, nazidharau, nami sitapendezwa na makutano yenu ya dini. Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za unga, sitazikubali; wala sitaziangalia sadaka zenu za amani, na za wanyama walionona. Niondoleeni kelele za nyimbo zenu; kwa maana sitaki kuzisikia sauti za vianda vyenu. Lakini hukumu na itelemke kama maji, na haki kama maji makuu.

Listen to the radio broadcast of

Kitu Mungu Anachokitaka

Download audio file

Kama vile cho chote kile kinaweza kubadilishwa kuwa njia ya kuchuma fedha, Ukristo pia unaweza kuwa kama biashara.  Yaani mali ya makanisa baadhi yanashangaza mno.  Kwa hiyo ni rahisi wachaMungu kama wewe na mimi kushawishika na mfumo ule.

Labda unafikiri kwamba nimekuwa mkali, sindiyo?  Lakini kanisa la Ukristo duniani limekalia matriliyoni ya dola ukizingatia viwanja vyao na rasilimali zingine, sehemu yake yasitumiwa vizuri hata kidogo.  Nikisema ukweli, simu yangu imejaa matangazo ya kongamano hii, upigaji muziki ule, mkutano maalum pale, unabii fulani … na kadhalika.

Ni kweli, kanisa linahitaji rasilimali ili litende kazi ya Mungu.  Ni kweli, kuwa ni mikutano mbali mbali duniani kujifunza Neno la Mungu na kumwabudu ni muhimu.  Lakini ni rahisi mtu kupelekwa na utendaji kazi wa biashara ya Ukristo inayosababisha watu wajiinue na kupoteza dira wasipambanue tena mapenzi ya Mungu hasa.

Sasa, Mungu anataka nini?  Yafuatayo yanaeleza anachokitaka yeye:

Amosi 5:21-24  Mimi nazichukia sikukuu zenu, nazidharau, nami sitapendezwa na makutano yenu ya dini.  Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za unga, sitazikubali; wala sitaziangalia sadaka zenu za amani, na za wanyama walionona.  Niondoleeni kelele za nyimbo zenu; kwa maana sitaki kuzisikia sauti za vianda vyenu.  Lakini hukumu na itelemke kama maji, na haki kama maji makuu.

Haina makona mengi.  Umwabudu Mungu kutoka moyo wako wote.  Ishia imani yako katika upendo kwa kutenda haki na kuwa mwadilifu.  Usivutwe tena na shamrashamra.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.

We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy