... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kosa ni la Nani?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mithali 19:3 Upumbavu wa mtu hupotosha njia yake; na moyo wake hununa juu ya BWANA.

Listen to the radio broadcast of

Kosa ni la Nani?


Download audio file

Mimi nimewahi kufanya mambo ya upumbavu maishani mwangu.  Na wewe pia, si kweli?  Tunatamani kama tungeweza kuyafuta … lakini haiwezekani.  Labda bado unaishia matokeo ya matendo yale.

Hatupendi kukiri makosa yetu; hatupendi kukubali kwamba tumekosea wala kukubali kwamba mtazamo wetu pamoja na matendo yetu yametuletea maumivu makubwa, hata kuwaletea wengine maumivu.  “Nimekosea” ni jambo ambalo linatuwia vigumu kulikiri moyoni hususani kukiri wazi mbele ya watu wengine.

Ni rahisi kumlaumu mtu mwingine na kwa kuwa Mungu anatawala kila kitu, ni rahisi kumlaumu yeye.  Bwana, kwa nini uliruhusu yale yatokee?  Kwa nini hukunitazamisha?  Kwa nini uliniruhusu niharibu mambo?

Kwa mtazamo wa haraka-haraka inaeleweka.  Ndiyo maana watu wananuna juu ya Mungu (hata kama ni kwa kuuliza maswali kama hayo tu).  Kwa hiyo inabidi sasa tuchukue hekima ya kimungu na kukemea suala la lawama-lawama.  

Mithali 19:3  Upumbavu wa mtu hupotosha njia yake; na moyo wake hununa juu ya BWANA.

Tukichunguza mstari huo kwa lugha ya asili ya Kiebrania tunaweza kusema hivi … Upumbavu wa mtu ukimpelekea kwenye uharibifu, ndipo moyo wake unamkasirikia BWANA.

Angalia, Mungu ni Mungu ambaye hawezi kutikisika na hata kama tunamlaumu, hawezi kuangushwa hata kidogo.  Halafu, jazba ikishuka na tukijirudi, yeye ni mwaminifu na atatusamehe.  Lakini tupokee maoni sasa, tujirudi mapema kabla hatujaenda huko.

Matokeo ya upumbavu wetu si kosa lake yeye.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.