Kristo Atakuja Tena
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Yohana 3:2 Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo.
Kinachochanganya sana katika maisha, ni wakati mtu anafanya maamuzi fulani – mfano, kufunga ndoa, kufuata masomo fulani, kufunga mkataba wa ajira, au cho chote kile – hawezi kujua matokeo yatakuwa nini. Nadhani umewahi kupitia hatua hizi au mojawapo ,si kweli?
Nakumbuka miaka ishirini iliyopita, wakati nilifanya maamuzi kushiriki huduma hii ya Christianityworks (Ukristou nafanyakazi kwelikweli), huduma inayowaletea kila siku vipindi hivi vya NENO SAFI NA LENYE AFYA. Yaani ilikuwa maamuzi yasiyoeleweka kwa sababu huduma hii ilikuwa inataka kufa kabisa.
Lakini kuna kitu kilinisukuma kujitolea.
Mashaka niliyokuwa nayo ndiyo yanaweza kuwasumbua watu wengi wanaokata shauri la kumwamini Mungu – hata wakiwa kwenye hatua gani. Yeye anaahidi baraka nyingi sana, lakini bado maisha ni mapambano tu.
Mtu anajaribu kuishi vizuri iwezekanavyo. Mara ingine, mtu anajikuta anazurura bure, akijiuliza kama Mungu yupo kweli kweli au la. Swala hili litaishaje?
Kama wewe una mashaka kama hayo, basi sikiliza vizuri, rafiki yangu, kwa sababu …
1 Yohana 3:2 Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo.
Hivyo ndivyo swala hili litaishia kwa kweli.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.