Kuangalia Yaliyo Mbele
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wafilipi 3:13,14 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.
Kwa kweli tunakaribia kufunga mwaka huu, inabaki leo na kesho tu, halafu mwaka mpya utaanza. Kwa hiyo muda umefika wa kusahau yaliyo nyuma na kulenga yaliyo mbele. Kwa kuwa nani anajua amebakiza miaka mingapi?
Niambie basi, umebakiza miaka mingapi wewe? Sasa, unataka kuitumiaje, huu muda mfupi unaobaki kwa maisha yako hapa duniani? Kwa kweli, haipaswi hata kidogo kuendelea kuishi tukiangalia yaliyopita – mtu akitamani siku za kale ambazo anazitaja kuwa bora, wala kugaagaa katika maumivu, makosa na majuto ya miaka ilizopita.
Kama tumekuwa pamoja siku hizi, tulishaona Mtume Paulo aliyewahi kuwa mtu wa kulitesa kanisa na tuliona kwamba alikuwa na majuto makubwa kuliko watu wengi. Lakini badala ya kuangalia nyuma, alifanya tofauti. Yeye mwenyewe alieleza hivi:
Wafilipi 3:13,14 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.
Rafiki yangu, muda umewadia kuachana na mwaka uliopita, hata mwaka juzi na zingine zilizotangulia. Kwa kweli, muda umewadia kabisa kabisa kusahau yaliyo nyuma na kulenga yaliyo mbele yako kwa sababu ya yale yote Yesu amekutendea. Usahau yaliyopita, halafu piga mbio ukilenga kumaliza vizuri katika mashindano na kupata tuzo yako ya ajabu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.