Kudhibiti Mawazo
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mithali 9:10 Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima; na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.
Hofu ni hisia ambayo hatufurahii. Hata kidogo! Kwa kweli, kama ingewezekana, tungeiepuka maisha yetu yote. Lakini kuna wakati mawazo yetu na hisia zetu vinatupelekea kwenye hofu.
Siku hizi kuna mawazo mengi mbali mbali, maoni na imani mbali mbali – tena mengi si sahihi, mengine ni ya hatari hata kuleta madhara.
Vyombo vya habari vinaegamia upande fulani, ujumbe wa biashara unaotuvuta kuachana na pesa tulizozihangaikia na mambo mengine ya ajabu-ajabu yanayozunguka-zunguka kwenye mtandao yasiyo na uthibitisho wo wote …
Sasa, mtu akitawaliwa na hayo yote, lazima ataingiwa na hofu.
Mithali 9:10 Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima; na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.
Kitu ambacho kinachohitajika kwetu, wewe na mimi, katika ulimwengu huu, mahali ambapo mawazo yasiyothibitishwa yanayotaka kututeka ni kimoja tu. Tunahitaji hekima. Hekima safi, hekima ya kweli na yenye upendo itokayo kwa Mungu.
Hekima hiyo tunaipata kwa kumcha Mungu, yaani kumheshimu yeye na njia zake, maagizo yake na maneno yake kuliko kinachoitwa hekima ya dunia hii.
Sio rahisi. Falsafa za dunia zinatusonga zikionekana tamu mwanzoni lakini chungu baada ya kumeza. kama vile Charles Spurgeon alivyowahi kusema, anayemwogopa Mungu hawezi kuogopa kitu kingine.
Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima; na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.