... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kufa Kila Siku Kwa Ajili ya Kristo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wagalatia 2:20 Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.

Listen to the radio broadcast of

Kufa Kila Siku Kwa Ajili ya Kristo


Download audio file

Tukisema ukweli kabisa, mambo mengi tunayoyatamani hapa duniani yanatokana na ubinafsi wetu tena hayana mwelekeo … mengine ni mabaya matupu.  We kubali tu, nivigumu kukomesha ubinafsi.

Hivi,  umewahi kutaka kumlipiza kisasi mtu kwasababu amekusumbua sana?  Au je!  Umetamani kuwa na pesa zaidi wakati unazo za kutosha na unamfahamu mtu ambaye anahitaji msaada wako?….nafikiri umeshanielewa.

Tuna matamanio mengi yanayoonekana kuwa mazuri kwa mtazamo wa haraka haraka … hadi pale unapogundua kwamba yote yanahusu “mimi”.  Ninachokitaka mimi, matamanio yangu mimi.  Halafu ulimwengu huu unaendelea kukusukuma ukisema, Kwa kweli unastahili hicho kitu.  Kinakufaa kabisa.  Nenda ukishikilie.

Kwahiyo, ule ubinafsi unatawala maisha yetu. Yamkini unamwamini Yesu lakini bado uko mtu yuleyule.  Unataka unachotaka na lazima ukipate. 

Mtume Paulo yeye, anatuonyesha njia tofauti kabisa.

Wagalatia 2:20  Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.

Kusulubiwa ni jambo la hatari.  Linahusu kufa kwa nafsi yako mwenyewe na kuishi kwa ajili ya Kristo.  Kumbuka pia kwamba Yesu alisema kwamba mtu akitaka kumfuata ajitwike msalaba wake, si mara moja tu, bali ni kila siku.

Kama vile mtu mmoja alivyowahi kusema, Lazima ufe kwa nafsi yako kila siku ili uweze kumwishia Kristo kikamilifu.  Ndipo ungeweza kusema pamoja na Paulo … wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy