kugeuzwa tabia
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Warumi 12:2 Wala msiifuatishe namna ya duni hii; bali mgeuzwwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Nina uhakika kwamba wewe, kama vile wengi wetu, una mambo kadhaa katika tabia yako ambayo ungependa kuyabadilisha. Ungependa kuwa mtu bora katika hili au lile. Lakini kama vile watu wengi, ulijaribu na ukafeli, yaani hukuweza kuleta mabadiliko kama ulivyotaka.
Vipepeo ni viumbe vinavyovutia sana. Kuna aina ya vipepeo 18,000 duniani vikiwa na rangi tofauti tofauti ya ajabu, tena vina umbo na saizi mbali mbali. Aina zingine kama vile kipepeo kiitwacho Monarch, vinasafiri maili maelfu kutoka Marekani ya Kaskazini hadi Mexico na kurudi tena kila mwaka. Vingine vinaishi wiki chache tu, halafu vinakufa.
Lakini vyote vinafanana kwa hili: Kila kipepeo kinaanza maisha kama kiwavu ambacho hatimaye kinakuwa na ugeuzaji wa umbo wa ajabu kabisa ndani ya kifukofuko kupitia mchakato unaoshangaza mno kuliko mabadiliko yote katika uumbaji. Sasa ugeuzaji wa tabia wenye nguvu kama vile kipepeo, ndio mfumo Mungu aliuandaa kwa ajili yako.
Warumi 12:2 Wala msiifuatishe namna ya duni hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Anachoeleza Mungu hapa ni kwamba wakati tunajaribu kujibadilisha, hatuwezi kabisa. Mwishowe tunafanana na watu wote wengine. Lakini tukimruhusu yeye kutubadilisha kwa ndani ,basi tutaweza kuishia maishi yale ya ajabu aliyokusudia kwa ajili yetu. Rafiki yangu, umruhusu Mungu kukubadilisha kuanzia ndani.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.