... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuielewa Neema

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 2:17-19 Walipomwona wakatoa habari waliyoambiwa juu ya huyo mtoto. Wote waliosikia wakastaajabu kwa hayo waliyoambiwa na wachungaji. Lakini Mariamu akayaweka maneno hayo yote, akiyafikiri moyoni mwake.

Listen to the radio broadcast of

Kuielewa Neema


Download audio file

Ni jambo zuri sana kuwa na kumbukumbu ya siku uliyompokea Yesu, na kama umeshampokea Yesu kama mimi, basi hongera sana, Lakini kuelewa kilichotokea kwa upana wake, hilo ni jambo lingine sasa.

Siku zimezopita kidogo tumekuwa tukitafakari kuhusu wale wachungaji namna walivyokuwa wametulia usiku ule baada ya kazi ngumu ya kuchunga kondoo zao.  Ghafla, wakatokewa na utukufu ukawang’aria pande zote, jeshi la mbinguni likitukuza jina la Bwana na kusema hosanaa!! … yaani, ni tukio la ajabu!, lakini pia tuliona muitikio wao. 

Wakakimbia ili wapate kumuona Yesu kwenye hori chafu la ng’ombe kama walivyoambiwa na malaika. Waliingia kwenye zizi wakiwa wameishiwa pumzi, na kusababisha Mariamu na Yusufu kujiuliza kinachoendelea. 

Luka 2:17-19  Walipomwona wakatoa habari waliyoambiwa juu ya huyo mtoto.  Wote waliosikia wakastaajabu kwa hayo waliyoambiwa na wachungaji.  Lakini Mariamu akayaweka maneno hayo yote, akiyafikiri moyoni mwake.

Ebu fikiria ilivyokuwa.  Mariamu amejifungua muda si mrefu, bado anamaumivu na bado anajisafisha.  halafu taarifa za ajabu zinakuja walizotangaza malaika.  Tayari Mariamu alijua kwamba mtoto wake si wa kawaida.  Lakini ufunuo huo ulimpa kutafakari mengi sana.  Mariamu akayaweka maneno hayo yote, akiyafikiri moyoni mwake. 

Kukumbatia neema ya Mungu kwako ndani ya Yesu Kristo si kazi ndogo ya dakika tano tu. inachukua maisha yote na hata kuendelea ili mtu aweze kuelewa ukubwa wa neema ya Mungu kwake.  Usiache kutafakari mambo hayo.  Usiache kujaribu kuyaelewa. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy