kuishi ndani ya Kristo …
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Yohana 3:4-6 Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi. Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake. Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua.
Ni jambo gumu sana kujaribu kuweka kichwa cha mzee mabegani mwa kijana; yaani kuwapa vijana wetu busara sisi wazee tuliojifunza kupitia changamoto za maisha kwa njia vijana wanayoweza kukubali.
Mimi ninakumbuka mambo mengi ambayo wazazi wangu walijaribu kunifundisha lakini nikayalaumu kwa kelele nyingi. Kwa hiyo ilibidi walazimishe ili waweze kunidhibiti. Mambo ya kawaida tu, kama vile kupanga chumba changu vizuri kiwe safi, kuchana nywele asubuhi kabla ya kutumia chai, kutokupinga agizo lao … na kila mara sikutulia bali nilinung’unika na kuendelea na hali yangu ya utoto.
lakini kumbe! Yameniletea matunda mema maishani mwangu mara tena na tena.
Na leo, ndivyo watu wanakataa kabisa dhana inayoonekana kwamba imepitwa na wakati, kwamba haiwahusu. Ni dhana ya dhambi. Ukitamka neno lile dogo, watu watakulalamikia mara moja. Je! wawezaje kuthubutu kunihukumu mimi? Wawezaje kujaribu kunilazimisha nikubaliane na imani yako iliyopitwa na wakati?
Mimi sitaki kumlazimisha mtu awaye wote. Nataka tu kukushirikisha kwa uwazi Neno la Mungu kama lilivyo:
1 Yohana 3:4-6 Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi. Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake. Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua.
Haijalishi wewe ni nani, haijalishi umefikia wapi maishani, tafadhali sana, usichezee swala la dhambi.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.