Kukubali Neno la Mungu Kama Lilivyo … au La
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yeremia 17:5,6 BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake na moyoni mwake amemwacha BWANA. Maana atakuwa kama fukara nyikani, hataona yatakapotokea mema; bali atakaa jangwani palipo ukame, katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.
Kwa mtazamo wa haraka-haraka, ni kama kuna vipengele vingi ndani ya Neno la Mungu ambavyo vinaonekana vinaenda kinyume na dhana za kisasa. Ikitokea hivyo, basi inabidi tuamue, wewe na mimi ni upande gani tutakaoufuata.
Ni changamoto ambayo sisi sote tunapambana nayo. Kuna pointi nyingi sana pale ambapo Maandiko yenye pumzi ya Mungu yanapopingana na fikra za jamii za sasa na mawazo yao kuhusu maadili; na hali hii inatuacha wewe na mimi tukivutwa huku na huko kila siku.
La kwanza kujua ni kwamba, hali hiyo si jambo jipya hata kidogo. Mara nyingi tunafikiri kwamba tukio kama hilo limetutokea sisi tu wa kizazi chetu. Lakini kuna sababu za watu wa Mungu kuteswa tangu enzi za kale. Ni kwa sababu upendo wa Mungu na njia zake na kweli yake vyote vinasimama kinyume na uovu uliopo duniani. Ndio maana walimsulubisha Yesu. Ndio maana Wakristo wamedhihakiwa na hata kuuawa tangu wakati ule.
Pia, zamani wakati wa Agano la Kale, wakati Israeli wanachagua njia isiyofaa, Mungu alikuwa na ya kuwaambia. Sikiliza vizuri:
Yeremia 17:5,6 BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake na moyoni mwake amemwacha BWANA. Maana atakuwa kama fukara nyikani, hataona yatakapotokea mema; bali atakaa jangwani palipo ukame, katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.
Ni rahisi sana kukosea, kama vile walivyofanya Israeli pale maneno yale yaliyoandikwa, wakipendelea hekima ya ki-dunia kuliko Neno la Mungu. Lakini kama vile mhubiri na mwinjilisti Mwingereza aitwaye Charles Spurgeon alivyosema: Roho Mtakatifu anatembea ndani ya gari nzuri la Maandiko si ndani ya mkogoteni wa mawazo ya kisasa ya binadamu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.