Kukubali Ukosoaji Unaojenga
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mithali 15:31 Sikio lisikilialo lawama yenye uhai litakaa kati yao wenye hekima.
Kama tulivyochunguza jana, kuna aina mbili tofauti za ukosoaji unaolingana nguvu na hatuna budi kukumbana nazo katika maisha. Aina ya kwanza unabomoa, ya pili unatujenga.
Ni kweli, kuna watu wanataka kukukatisha tamaa na kukuchelewesha na kukuyumbisha. Hata kwetu wapo. Kwa kukabiliana nao, inabidi mtu atumie utambuzi.
Lakini mara nyingi ukosoaji unatoka kwa watu wanye nia njema, watu wanaojali hata kama ukosoaji wao unatuumiza. Hata kama wao wenyewe hawauleti vizuri kama inavyopaswa. Hata kama ukosoaji wao unakuwa kama hukumu, au wanauleta kwa muda usiofaa, ao ni kama wanatusumbua tu. Pengine sauti yao au sura zao zinachukiza na kusababisha tusipokee maneno yao ya hekima.
Mithali 15:31 Sikio lisikilialo lawama yenye uhai litakaa kati yao wenye hekima.
Hata kwa hali hiyo, bado utambuzi unahitajika. Tusiangalie sana kama tuko tayari kupokea ukosoaji wao, au labda umechokoza kiburi chetu au labda wameuleta vibaya. Swali la msingi ni kuuliza, Je! Ukosoaji huu utanisaidia? Nikiusikiliza, Je! Utanisaidia nini katika maisha yangu? Hapo ndipo mtu anaweza kutambua kama itamfaa kuupokea au la.
Kwa kuwa, Sikio lisikilialo lawama yenye uhai litakaa kati yao wenye hekima.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.