... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kulenga Upya Uone Vizuri

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mariko 12:29-31 Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.

Listen to the radio broadcast of

Kulenga Upya Uone Vizuri


Download audio file

Kumbe!  Tayari ni tarehe ya tisa ya mwaka mpya.  Mambo bila shaka yamerudi kuwa ya kawaida.  Kila mmoja ameendelea na shughuli zake.  Lakini acha nikuulize, Je!  Umerudia taratibu zile zile, kama vile gari halina budi kufuata alama za magurudumu ya magari yaliyotangulia katika tope?  Ikiwa hivyo, je!  Unaweza kutazamia kwamba mambo yatakuwa tofauti na hatimaye kuwa bora kweli?

Dhana hiyo labda inaweza kumkatisha tamaa mtu, !!!Kama vile wanavyosema, kurukwa na akili ni kufanya jambo fulani tena na tena, mtu akitazamia kupata matokeo tofauti.  Lakini tukisema wazi, wengi wetu hatutaki kubadilika.  Mtu anafarijika akistarehe katika mambo aliyoyazoea au akitembea katika njia ile ile hata kama si njia iliyo bora.

Ni kama utambulisho wetu umeambatana na jinsi tulivyokuwa tunafanya mambo mbali mbali kwa muda mrefu na sasa, kuleta mabadiliko – hata yakiwa madogo – inaashiria kwamba tulikuwa tumekosea muda ule wote.

Kwa hiyo, niruhusu nikuulize, je!  Unalenga nini kwa upya mwanzo wa mwaka huu mpya?  Utashikaje hisia kwamba maisha yako yana maana iwezayo kukuridhisha, hali uliyoshindwa kufikia muda mrefu?

Mariko 12:29-31  Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.  Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.  Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy