... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuleta Amani

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Tito 2:1-5 Lakini wewe nena mambo yapasayo mafundisho yenye uzima; ya kwamba wazee wawe wenye kiasi, wastahivu, wenye busara, wazima katika imani na katika upendo na katika saburi. Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema; ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao; na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe.

Listen to the radio broadcast of

Kuleta Amani

Download audio file

Swali:  Je!  Vita vinaishaje?  Jibu:  Baada ya mapigano makali, na maafa ya watu wengi pande zote mbili, hatimaye wanakubali kuketi mezani na kujadili swala la amani.  Ninachotaka kusema ni kwamba amani haitokei hivi-hivi tu.

Leo hii, kuna migogoro mingi inayoendelea katika jamii – siasa ya jinsia, matajiri dhidi ya maskini, weusi dhidi ya weupe.  Migogoro haipo katika jamii tu, ni ndani ya maisha yetu, familia zetu hapo hapo tunapoishi.

Ni kwa sababu gani?  Ni kwa sababu tumeenda mbali na maarifa ya kawaida, tumeenda mbali na hekima ya kimungu, Pia, ni kwa sababu tumejifanya kuwa watu wanaojua kila kitu.  Kwa hiyo sikiliza maarifa ya kawaida yanayotoka … kwa Mungu mwenyewe:

Tito 2:1-5  Lakini wewe nena mambo yapasayo mafundisho yenye uzima; ya kwamba wazee wawe wenye kiasi, wastahivu, wenye busara, wazima katika imani na katika upendo na katika saburi.  Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema; ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao; na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe.

Ni kweli, mambo mengine yamebadilika, lakini sisi sote, vijana kwa wazee, kila mmoja wetu anaajibika kuleta amani katika familia zetu, rafiki zetu na jumuia.  Najua kwamba si rahisi.  Ni kujitahidi na kujitolea.  Hekima inahitajika.  Lakini amani haitokei hivi-hivi tu.  wajibika na sehemu yako ili na wewe uchangie kuleta amani.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.

We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy