... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuliko Yote Uyawazayo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waefeso 3:20,21 Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina.

Listen to the radio broadcast of

Kuliko Yote Uyawazayo


Download audio file

Ukiangalia yote yanayoendelea katika moyo wako na fikra zako, ukizingatia pia yanayoendelea maishani mwako au katika ulimwengu unaotuzunguka, je!  Kuna wakati unajisikia … kwamba huna nguvu? Hata kidogo?  Sio wewe tu peke yako.

Hata mimi, kuna wakati ninajisikia kwamba sina nguvu kabisa.  Hua inatutokea sisi sote.  Tunakabiliana na mambo yanayotuzidi sana, hadi pale tunatishiwa kwamba tunaweza kumezwa nayo.

Jana tuliongea habari ya nyota ma-triliyoni huko mbinguni.  Leo nataka tuchunguze habari ya nyota moja tu – yaani jua letu.  Kila sekunde, jua linazalisha uwezo wa 384.6 septilioni za wati.  Kwa maelezo mengine, ni uwezo unaozidi bomu ya nukliari kubwa uliopo kuliko mara biliyoni.

Lakini jua letu, si nyota kubwa sana katika nyota ma-triliyoni tunazojua zilizopo.  Na Mungu aliziumba zote.  Kwa hiyo mtu akiongea habari ya uweza wake Mungu, lazima awaze yaliyo makuu kabisa.

Waefeso 3:20,21  Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina.

Wakati tumeishiwa nguvu, Mungu ana nguvu izidiyo – sana sana ya kutosha – uwezo wa kutusaidia kukumbana na yo yote yale tunayokabiliana nayo.  Sasa, uwezo huo – uwezo wake – ukifanya kazi ndani yetu, yeye anaweza kufanya mambo ya ajabu mno kuliko tuyaombayo au tuyawazayo.

Sasa ikitokea hivyo … basi, utukufu umrudie yeye.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.