Kumbukumbu Iokoayo
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Petro 3:11,12 Na aache mabaya, atende mema; atafute amani, aifuate sana. Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake husikiliza maombi yao; bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya.
Mema na mabaya – sisi sote tunaweza kuyatenganisha … au? Ni kama kutenganisha rangi nyeusi na rangi nyeupe, ni rahisi sana … au labda tunapendelea rangi fulani ya katikati ya kijivu? Wewe unaonaje?
Yaani, mambo yako hivi. Wakati tunahukumu matendo ya watu wengine, kwa kweli tunachunguza yaliyo meusi na yaliyo meupe katika maneno na mambo wanayofanya au kushindwa kufanya.
Lakini kuhusu sisi wenyewe kwa kujihukumu – mawazo yetu, makusudi yetu, maneno yetu na matendo yetu – mara nyingi hatuyafikirii sana; hatujihoji na hata kama tunajipima mara ingine, tunapaka chokaa juu ya mengi yaliyo myeusi.
Je! Kuna kosa lo lote katika kuchanganya kidogo myeusi na myeupe?
Lakini kwa Mungu, mambo yako dhairi tu, au ni habari njema au habari mbaya, inategemeana mtu anakaa pande gani.
1 Petro 3:11,12 Na aache mabaya, atende mema; atafute amani, aifuate sana. Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake husikiliza maombi yao; bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya.
Sisi sote tuna mwelekeo wa kuruhusu maafikiano na ubaya kuingia maishani mwetu, na bila hata kujua, amani tuliyokuwa nayo yanatoweka. Baraka zile ambazo Mungu alikuwa anatukirimia kwazo, kumbe! Hazipo tena, wala hatupati majibu ya maombi yetu kama yalikuwa yanatiririka hapo awali. Kuna sababu iko hivi.
Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake husikiliza maombi yao; bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.