... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kumkaribia Mungu au Kujitenga Naye

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 73:27,28 Maana wajitengao nawe watapotea; umewaangamiza wote waliokuacha wewe. Nami kumkaribia Mungu ni kwema kwangu; nimefanya kimbilio kwa Bwana MUNGU, niyahubiri matendo yako yote.

Listen to the radio broadcast of

Kumkaribia Mungu au Kujitenga Naye


Download audio file

Gari zinazoendeshwa na umeme zinaanza kupendwa na kuenea duniani.  Ni sawa, ila mimi, nikifadhaishwa wakati simu yangu imeishiwa moto, kwa kweli nina mashaka kuhusu gari ya umeme kuniisihia chaji safarini.  Sijui wewe unaonaje?

Ni kweli, gari ya umeme kuishiwa chaji haina tofauti na gari ya kawaida kuishiwa petroli.  Kukwama kwa zote mbili kunatokana na ukweli huu usioepukika:  Mtu akienda mbali na chanzo cha nishati yake kwa muda mrefu, lazima ataishiwa nguvu na kusimama.

Na maisha ndivyo yalivyo.  Jana tulisimulia kwamba mtu akianza kukomaa, ndipo atazidi kutokuendelea kujitegemea akizidi kuelewa madhaifu na mapungufu yake.  Mwili na moyo hua unapunguka, lakini Mungu anaweza kuwa nguvu ya mioyo yetu na sehemu yetu milele.

Ni habari njema.  Habari njema mno.  Lakini haitasaidia mtu akimwacha Mungu kwenda mbali kwa muda mrefu:

Zaburi 73:27,28  Maana wajitengao nawe watapotea; umewaangamiza wote waliokuacha wewe.  Nami kumkaribia Mungu ni kwema kwangu; nimefanya kimbilio kwa Bwana MUNGU, niyahubiri matendo yako yote.

Watu wengi wanaokiri kuwa na imani ndani ya Mungu, wanamwacha kwa muda mrefu wakienda mbali naye.  Labda umejitenga naye.  Kama ndiyo hali yako, basi jua neno hili:  Maana wajitengao nawe watapotea; umewaangamiza wote waliokuacha wewe.   

Bali kwangu mimi kumkaribia Mungu ni kwema kwangu; nimefanya kimbilio kwa Bwana MUNGU, niyahubiri matendo yako yote.

Umkaribie Mungu.  Usijitenge naye.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy