... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuna Imani ya Uchawi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Yohana 3:8 Atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.

Listen to the radio broadcast of

Kuna Imani ya Uchawi


Download audio file

Leo ni siku ya Ijumaa tarehe 13.  Siku ile na tarehe ile zikikutana, katika utamaduni wa magharibi, zinadhaniwa kuleta bahati mbaya.  Haijalishi unaishi wapi, ushirikina na uchawi umekuwepo tangu karne za kale – mfano: usipite chini ya panda ngazi iliyowekwa ukutani, ole kwako ukiona paka mweusi anapita mbele yako au ukivunja kioo utapata bahati mbaya kwa miaka saba.  Haya yote yanasemekana kwamba yanaleta bahati mbaya.

Ukitafakari kidogo, utagundua kwamba mzizi wa ushirikina ni hofu.  Na hofu ambayo ni hisia mbaya kuliko zote, mara nyingi inatokana na uovu – sisemi hofu zote, lakini hofu tunayozung’mzia leo.

Ebu fikiria, woga kamwe hautokani na upendo, wema, huruma, au kutenda haki, lakini unatokana na uovu – ukatili, kiburi, ubinafsi na kadhalika.  Akina mama wengi sana na watoto wasiohesabika wanaishi katika hali ya hofu kabisa sababu ya ukatili wa wanaume nyumbani mwao.

Karibia watu wote wanaamini kwamba kuna sehemu ya kiroho katika maisha ya mwanadamu.  Na tusidanganyike, sehemu hii ya kiroho ina sehemu mbili, wema na uovu.

1 Yohana 3:8  Atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo.  Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.

Rafiki yangu, usimruhusu Shetani kuvuruga maisha yako.  Usimruhusu akuvute kutenda mabaya, usimruhusu kuleta giza na hofu maishani mwako, kwa sababu kuna njia mbadala.  Ni Yesu aliyekuja ili azivunje kazi za Ibilisi … maishani mwako.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy