Kungoja Tofauti
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 27:13,14 Naamini ya kuwa nitauona wema wa BWANA katika nchi ya walio hai. Umngoje BWANA, uwe hodari, upige moyo konde, naam, umngoje BWANA.
Je! Unapenda sana kungoja hadi mambo yatokee? Ikiwa Jambo jema, au jambo la muhimu, au jambo ambalo umekuwa na shauku nalo muda mrefu, au jambo ambalo ni lazima litokee au itakuwa balaa. Je! Kuvuta subira kunakupendeza kiasi gani?
Nadhani jibu la swali hilo, kwa kawaida na kwa karibia watu wote ni … hatupendi kabisa. Wakati unahitaji kusonga mbele licha ya upinzani, unataka itokee mara moja! Wakati unahitaji uponyaji, sasa hivi ingekuwa muda mwafaka, si kweli? Wakati mtu anateswa, anataka yaishe SASA HIVI! Lakini kwa kawaida, mambo hayatokei hivyo.
Kamusi yangu inaniambia tafsiri ya kungoja. Ni kubaki sehemu uliopo au kusubiri usitende lo lote hadi muda fulani au kitu fulani kitokee. Na kusubiri si rahisi wakati wewe unataka kusonga mbele.
Daudi, akiwa hatarini akiwindwa na watu hata na jeshi wakitaka kuangamiza uhai wake. Katika zaburi alisema haya..
Zaburi 27:13,14 Naamini ya kuwa nitauona wema wa BWANA katika nchi ya walio hai. Umngoje BWANA, uwe hodari, upige moyo konde, naam, umngoje BWANA.
Aliwezaje kusubiri? Kwa kuamini kwamba, kabla hajafa, atauona wema wa Mungu kwa macho yake yenyewe,
Kwa sababu Bwana ni mwema, kila wakati … lakini anatenda kufuatana na ratiba yake yeye.
Umngoje BWANA, uwe hodari, upige moyo konde, naam, umngoje BWANA.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.