... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kupita Ufahamu Kabisa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mariko 2:15-17 Hata alipokuwa ameketi chakulani nyumbani mwake, watoza ushuru wengi na wenye dhambi waliketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake; kwa maana walikuwa wengi wakimfuata. Na waandishi na Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? Yesu aliposikia aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.

Listen to the radio broadcast of

Kupita Ufahamu Kabisa

Download audio file

Ingekuwaje kama mtu tajiri au mwenye mamlaka – mfalme au mwimbaji maarufu au mtu mashuhuri au mtu anayejulikana sana – kama angefika ili ale nyumbani mwenu?  Nijibu, ungeonaje?

Jana tuliona jinsi mtoza ushuru Lawi – mtu aliyekataliwa na wananchi wenzake – alivyoitwa na mwalimu maarufu aitwaye Yesu, jambo la kushangaza mno.  Sasa mambo yanazidi kushangaza kwa sababu …

Mariko 2:15-17  Hata alipokuwa ameketi chakulani nyumbani mwake, watoza ushuru wengi na wenye dhambi waliketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake; kwa maana walikuwa wengi wakimfuata.  Na waandishi na Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?  Yesu aliposikia aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.  

Ni kweli, Yesu alipenda kukaa na waliotengwa, makahaba na walevi.  Lakini hakuja kuwabembeleza wala kuunga mkono dhambi zao, hapana.  Kwa sababu baada ya wao kukaa naye, hawakuwa tena watu wa kutengwa wala makahaba wala walevi.

Uwepo wa Kristo mezani unaweza kubadilisha maisha ya mtu mara moja.  Hata maisha yako wewe na mimi.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.

We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy