... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kupofushwa Kwa Kutokujali Kweli

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 8:31,32 Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.

Listen to the radio broadcast of

Kupofushwa Kwa Kutokujali Kweli


Download audio file

Sijui kama umeshawahi kutamani kitu fulani kiwepo hadi ukawa tayari kufanya chochote ili kitu hicho kiwepo?  Huwa inatutokea mara nyingi tu, lakini mtu akiendea njia hiyo atakuwa amejiingiza hatarini.  

Kulikuwa na Daktari aitwaye William McBride aliyekuwa daktari bingwa wa uzazi huko kwetu Australia, alikuwa maarufu kwasababu mwaka 1961 aligundua kuwa; dawa ya thalidomide iliyokuwa inatolewa wakati ule kwa wajawazito, ilikuwa inasababisha dosari ya kimaumbile kwa watoto waliokuwa wanazaliwa.  Yaani, alipongezwa sana kwa utafiti wake.  Lakini mwaka 1989 alihukumiwa kwa kosa la ulaghai wa kisayansi kwa matokeo ya utafiti mwingine wa tiba.  

mahakama ya tiba iligundua kuwa, “Daktari McBride alijaribu kuficha udanganyifu wake … Je!  Tukio kama hilo linatokana na nini?  Linaweza kutokea kwasababu mtu anataka kitu kiwe cha kweli hata kama si kweli, kwa hiyo atafumba macho yake asione mambo halisi.

hali kama hiyo inatokea mara nyingi leo, hususani miaka hii miwili iliyopita kwenye swala la janga la Corona, unakuta tabaka fulani katika jamii limeshikilia maoni ya kundi lao na kufumbia macho ukweli, kisha kusababisha watu wengi kupoteza maisha bila hatia, 

Shida inatokana na watu ambao kwa upande mwingine wanaonekana kama wenye akili, lakini wanasukumwa na nia ya hovyo kutaka kuthibitisha matokeo wanayoyataka wao, licha ya ukweli wa data unavyoeleza. 

Yesu, katika mazingira tofauti, aliweza kuleta kanuni ifuatayo: 

Yohana 8:31,32  Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru. 

Ni kanuni gani?  Lazima ujue ukweli uko wapi ili uweze kukuweka huru.  Usijifanye mtu asiyejali  ukweli. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy