Kutawaliwa na Jeuri na Hali ya Kuchukizwa Daima
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Tito 3:1,2 Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema; wasimtukane mtu ye yote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote.
Kutawaliwa na Jeuri na Hali ya Kuchukizwa Daima
Download audio file
Je! Unaonaje? Wanaotawala nchi yako, au mkoa wako au wilaya yako, au kijiji au mji wako, wakoje? Kwa mtazamo wako, je! Wanatawala vizuri … au kama vile watu wengi, unachukizwa na mienendo yao?
Leo, kuna watu wengine watakaotafakari maswali yangu mahali ambapo hawana uhuru wa kutoa maoni yao. Lakini kwa wengine wengi, hawasiti kueleza wanavyochukizwa na sera zisizoeleweka na mienendo ya viongozi baadhi. Wanachukizwa na jinsi viongozi wanaovaa na kutamka, wanachukizwa na unafiki na ufisadi wao.
Juzi nilisoma kibainishi kiitwacho, “Je! Tumetawaliwa na Jeuri?” Hoja yake ni kwamba tumezoea kukwazika na kuchukizwa. Ukitafiti mada hii, utaona kwamba ni mada inayozung’mzwa sana siku hizi, kuanzia wanasaikolojia hadi gazeti za mitindo.
Kuna nadharia nyingi za njama. Halafu, kinachohuzunisha zaidi ni kuona jinsi watu wanaojiita “Wakristo” wako mstari wa mbele katika mgogoro huo. Muda umewadia wa kujihoji kwa kweli:
Tito 3:1,2 Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema; wasimtukane mtu ye yote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote.
Labda hautapendezwa na maneno hayo. Kwa sehemu ninakuelewa, lakini ujue kwamba …
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.