Kutembea Juu ya Ardhi Iliyo Imara
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Isaya 40:27,28 Mbona unasema, Ee Yakoko, mbona unanena, Ee Israeli, Njia yangu imefichwa, BWANA asiione, na hukumu yangu imempita Mungu wangu asiiangalie? Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.
Kwa kuwa tumeanza mwaka mpya … nadhani utakubaliana nami kwamba ni muhimu tuanze hatua ya kwanza vizuri kwa kukanyaga ardhi iliyo imara, si kweli? Kumbuka kwamba daima, kuweka msingi imara ni muhimu sana.
Je! Ungependelea kutembea juu ya ardhi iliyo imara au juu ya mchanga didimizi? Hata kama jibu ni rahisi sana, ni huzuni kuona jinsi watu wengi wanachagua kupita kwenye mchanga didimizi bila hata kufikiria. Inakuaje? Ni kwa sababu tunapiga hatua ya kuingia mwaka mpya tukitegemea kwamba matumaini na matazamio yetu yote yatatimia mwaka huu; kwamba maisha yatakuwa mazuri na watu watatutendea haki, kwamba mwaka huu tutakuwa na afya, tutapata mali na tutazidi kuwa na hekima.
Halafu ghafla, msiba unajitokeza, kuna hasara kubwa, dhoruba inatujia. Mwezi Aprili mwaka jana, kuna mtu aliyetenda jeuri na kuanza kuchoma watu kisu sokoni karibu sana na ofisi zetu tunapohudumia. Aliua watu saba na kujehuri wengine wengi. Hakuna hata mmoja angetazamia tukio hilo litokee. Hata mmoja!
Isaya 40:27,28 Mbona unasema, Ee Yakoko, mbona unanena, Ee Israeli, Njia yangu imefichwa, BWANA asiione, na hukumu yangu imempita Mungu wangu asiiangalie? Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.
Haijalishi mazingira yako yanatikiswa kiasi gani, Mungu ndiye mwamba imara. Daima amekuwa hivi. Na daima ataendelea kuwa hivi.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.