Kutembea na Uhodari
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
2 Timotheo 4:1-4 Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake; lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.
Namshukuru Mungu kwamba sikuwa Mkristo mhubiri, sijui ingekuwaje jamani, duh, kupaza sauti na hakuna anayesikiliza!, yaani nahisi ingekuwa vurugu! Lakini kwa njia moja ama nyingine, kila mtu anayemwamini Yesu ni mhubiri.
Kama tulivyoona jana, ukweli wa Neno la Mungu, ukweli unaohusu upendo wake, uadilifu wake, neema yake na huruma zake, yote yanashambuliwa vibaya leo hii kuliko ilivyokuwa zamani.
Mawazo ya Wakristo yanapingwa kwasababu hayaendi sambamba na sera za walimwengu. Inaonekana kwamba kila mtu ana mambo yake anayoyasukuma akiwa na agenda za ubinafsi anazotaka kutimiza. Katika mazingira magumu kama haya, ni rahisi mtu anayemwamini Yesu kwa moyo wake wote, kuruhusu Injili ya Kristo inyamazishwe.
Lakini wewe unafahamu na mimi pia ninafahaumu kwamba kweli inasababisha watu wastawi. Ukweli wa Mungu unaongoza watu kwenye uhuru. Sasa jibu litapatikana wapi? Leo nitanukuu tena maneno ya Mtume Paulo aliyomwambia kijana wake Timotheo, mwanafunzi wake, kuhusu mada hiyo:
2 Timotheo 4:1-4 Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake; lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.
Kumbe hali hiyo iliyokuwepo zamani inataka kufanana na namna mambo yalivyo leo, sindiyo? Sasa jibu linapatikana wapi? Jibu ni kutembea na ujasiri, kuwa na moyo mkuu kila wakati, kuwa tayari kuhubiri Neno wakati ukufaao na usiokufaa.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.