Kutoka Kwenye Majivu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Isaya 37:31-32 Na mabaki yaliyookoka, yaliyobakia ya nyumba ya Yuda, yatatia mizizi chini na kuzaa matunda juu. Maana katika Yerusalemu yatatoka mabaki, nao watakaookoka katika mlima Sayuni; wivu wa BWANA wa majeshi utatimiza mambo hayo.
Mmea uitwao mshubiri una sifa kwamba unaweza kutibu magonjwa mbali mbali na kurejesha hali nzuri ya ngozi. Labda ni kweli. Hata hivi, mtu anaweza kuwa na mashaka kwamba wafanyabiashara na watangazaji wao wanaweza kukuza nguvu wakijaribu kuongeza mapato na kuuza vipodozi ambavyo labda kuna sehemu ndogo sana ya mmea huo.
Wafanyabiashara mara nyingi wanafaulu kwa sababu dhana ya kurejeshewa hali ya ujana ni dhana yenye nguvu. Kama vile rafiki yangu mmoja wa zamani katika teknolojia alipenda kusema, Dhana ile inavuta fikra za watu, wakaziegesha pale pale.
Juzi nilishtuka mno, nikatishwa kabisa kwa sababu kuna mtu alinitaja katika barua pepe kuwa “mzee wa umri” – hata kama nikiwa na umri wa miaka 65, bado ninapendelea kupanda na kushuka ngazi kwa kasi badala ya kutumia lifti. Jamani! Niletee kipodozi cha mshubiri niweze kujipaka usoni!
Lakini tukiacha utani, sote tunahitaji kupata urejesho: wakati tunajisikia kwamba tumechoka sana, tumeishiwa nguvu na tunaweza kuvamiwa kwa urahisi;
Wakati adhabu ilikaribia kuangukia taifa la Israeli, jiji la Yerusalem lingechomwa moto na pangebaki majivu tu, Mungu aliwaambia hivi:
Isaya 37:31-32 Na mabaki yaliyookoka, yaliyobakia ya nyumba ya Yuda, yatatia mizizi chini na kuzaa matunda juu. Maana katika Yerusalemu yatatoka mabaki, nao watakaookoka katika mlima Sayuni; wivu wa BWANA wa majeshi utatimiza mambo hayo.
Chipukizi cha kijani kutoka majivu kikiwa na mizizi mirefu kwenda chini ambacho hatimaye kitazaa matunda mengi juu ya nchi …
Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.