Kutua Salama Salamini
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Ufunuo 5:8 Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.
Ninajiuliza wakati wewe unaomba – na watafiti wanatwambia kwamba karibu watu wote kuna mara wanaomba – je! Umewahi kujiuliza dua lako linaishia wapi? Mungu analipokeaje? Lina mtisiko gani?
Nahisi kwamba watu wengi hawajiulizi maswali kama hayo, bali wanarusha maombi yao huko wakibahatisha kupata matokeo mema. Je wewe binafsi, umewahi kujiuliza maswali hayo? Je! Umewahi kujiuliza maombi yako yanafananaje huko kwenye mazingira ya mbinguni?
Katika kitabo cha ajabu cha Ufunuo, Mungu anaainisha maombi yetu kwa jinsi ya ajabu:
Ufunuo 5:8 Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.
Maombi yetu yanafananishwa na vitasa vilivyojaa manukato mbele zake Yesu – yaani ni picha yenye utukufu ya jinsi maombi yetu yanavyopanda mbele zake. Lakini sasa tuulize, je! Yana mtikiso gani hapa duniani? Niliguswa sana na maneno rafiki yangu ambaye amekuwa mishonari maisha yake yote Afrika, Lowell Wertz alivyoandika hivi karibuni:
“Maombi ni mahusiano na Baba ambayo yanapokelewa vizuri naye, pia yanatufariji sisi wenyewe. Tunaomba kwa sababu tunamhitaji Mungu na tunampenda pia. Yeye anataka kusikia kutoka kwetu. Maombi yetu yanasikilizwa mbinguni. Kulikuwa wakati ombi langu kali sana lilisikilizwa nikiwa rubani mpya kabisa aliyekuwa anajaribu kutua ndege kwenye uwanja mwembamba wa udongo mahali fulani Afrika na dhoruba kubwa mno ulikuwa unapiga. Nilishindwa kuona mbeleni, na niliomba kwa kupiga kelele nikipaza sauti zaidi ya ngurumo ya enjini ya ndege na mvua. Roho Mtakatifu alijaa dungu la ndege nilimokaa na nilitua vizuri salama salamini.”
Ombi lako linapokelewa vizuri mbinguni na lina mtikiso hapa duniani pia.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.