... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuwa Kama Beethoven

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Petro 4:10,11 Kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu. Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina.

Listen to the radio broadcast of

Kuwa Kama Beethoven


Download audio file

Mara nyingi sana vipawa na vipaji kutoka kwa Mungu ambavyo viliumbwa ndani yetu, watu wengine hawavioni wala hawavithamini, tena isitoshe, watakwambia usifanye yale Mungu aliyokuitia uyafanye, wakileta sababu nyingi tu.  Nadhani umeshaona.

Hata kama hufuati sana muziki, inawezekana umeshasikia habari za mtunga muziki maarufu wa zamani aitwaye Ludwig van Beethoven.  Wakati bado anapiga hatua nzuri katika ustadi wake, ghafla alipatwa na ulemavu wa kuwa kiziwi.  Aliambiwa kwamba hataweza kutungu muziki tena. 

Je!, Ludwig aliwasikiliza?, Waala!  Cha ajabu sasa yeye baada ya kuwa kiziwi, aliweza kutunga nyimbo ya muziki bora kuliko zile za kwanza!  Na mimi, niliamua kuacha kazi yangu nzuri iliyonilipa sana katika fani yangu kuwa fundi stadi wa kutengeneza maswala ya mtandao, na kuingia katika huduma yetu hii iliyokuwa inayumba-yumba, watu wengi wenye nia njema walijaribu kunishawishi nisifanye uamuzi huo. 

Unaona, watu wengine mara nyingi hawawezi kutambua wito wa Mungu juu ya maisha yetu.  Kwao haieleweki, lakini wewe unauelewa.  Unafahamu vipaji na vipawa ulivyokirimiwa na Mungu.  Una shauku kuwa mtu yule aliyekusudia uwe, ukitaka sana kufuata wito wake kwa sababu … 

1 Petro 4:10,11  Kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.  Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo.  Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina. 

Kamwe usiruhusu ukosefu wa maoni ndani ya watu wengine kukuzuia usifuate wito wa Mungu juu ya maisha yako.  Nenda ukawa yote aliyekusudia uwe wakati alipokuumba. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy