... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuwa Karibu na Mtu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Warumi 12:15,16 Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao. Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.

Listen to the radio broadcast of

Kuwa Karibu na Mtu


Download audio file

Mtu ye yote aliyewahi kulea watoto anafahamu umuhimu wa kusherehekea mafanikio yao na kuwa karibu nao wakati wanaumia.  Tunafahamu hayo kwa sababu ni silika ya kibinadamu.  Lakini kwa nini ni muhimu?

Hakuna kitu kingine ambacho tunaweza kuchangia kwenye uhusiano fulani chenye nguvu na upendo kuliko uwezo wa kuhisi maono ya mwingine.  Unajenga daraja na ushirikano wa karibu kati ya watu wawili, umoja ambao ingekuwa vigumu kuuvunja.

Sasa, hata kama tunaelewa umuhimu wake maishani mwa watoto wetu, kwa njia moja au nyingine, kuna wakati tunasahau kwamba ni muhimu kwa watu wazima pia.  

Akiongea jinsi mtu anaweza kuishi maisha ya kumcha Mungu, Mtume Paulo aliandika hivi:

Warumi 12:15,16  Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao.  Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi.  Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge.  Msiwe watu wa kujivunia akili.

Maneno hayo yanaweza kusaidia kabisa, si kweli?  Ni sahihi kabisa.  Yanaweza kutusaidia muda huu huu.

Uwapende watu, uishi nao kwa amani, waonyeshe kwamba wewe huna kiburi kwa kukubali kuwa karibu nao katika kila hali, ukionyesha uwezo makuhusi kama wanavyohisi wakati wo wote, ukifurahi pamoja nao au ukilia pamoja nao.

Kwa hiyo leo, kesho, hata maishani mwako wote, kati ya marafiki, watu ambao unaofanya kazi nao, wapendwa na hata wageni … Furahi pamoja nao wafurahio; lia pamoja nao waliao.  

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.