... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuwa na Amani … au La

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Isaya 57:19 Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani, amani, kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema BWANA; nami nitamponya.

Listen to the radio broadcast of

Kuwa na Amani … au La


Download audio file

Kuna ukweli unaotisha kabisa:  Ulimwengu umepamba moto kwa sababu ya vita.  Miaka hii ya karibuni, kufuatana na tovuti OurWorldinData.org, mapigano ya vita 150 hua yanatokea kila mwaka.  Hii ni zaidi ya miaka ishirini, thelathini iliyopita lakini hata wakati ule, ni mara haba wastani wa mapigano ilikuwa chini ya 100 kila mwaka.  Ebu jaribu kutafakari hatari hiyo!

Siku hizi mapigano huko Ukraine na Mashariki ya Kati yamewekwa bayana na vyombo vya habari lakini bara la Afrika linaendelea kuwa uwanja wa vita kali hapa na pale – jambo ambalo halitangazwi sana na waandishi wa habari kwenye nchi za magharibi.

Yaani mateso yaliyosababishwa na vita yanaendelea kila siku tena yanapita ufahamu wetu.  Mtoto mmoja akiteswa vibaya, sembuse maelfu na maelfu.  Mwanajeshi mmoja kuuawa ni msiba, sembuse maelfu na maelfu wanaouawa kila siku!  Lakini sisi wengine tunaamka asubuhi, tunaoga na kutumia chai na kwenda kazini kama kawaida tu.

Lakini hata kama hali hiyo inatisha mno, kuna mateso yaliyo makubwa zaidi katika wanadamu wote – ni migogoro ambayo kila mtu anakabiliana nayo katika mahusiano yake na watu wengine. 

Isaya 57:19  Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani, amani, kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema BWANA; nami nitamponya.

Mungu anataka uweze kufahamu amani yake.  Anataka kukufundisha kuishi kwa amani.  Kwa mstari unaofuata, Isaya anasema kwamba hakuna amani kwa wanaoendelea kutenda maovu.

Tafadhali, usijiumize bure, bali jihurumie kwanza.  Achana kabisa na uovu uliomo maishani mwako.  Umsogelee Mungu siku baada ya siku halafu umruhusu akufundishe neno jipya: amani.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy