Kuwa na Jina Kuna Maana Gani?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Isaya 43:1 Lakini sasa, BWANA aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.
Sijui kama ni shida kwako kama ilivyo kwangu kukumbuka jina la mtu, hata kama ametambulishwa kwangu punde tu? Ni shida kweli. Lakini jina la mtu ni muhimu sana kwake yeye. Kwa hiyo, hata kama hatukukusudia, kulisahau jina la mtu inaonekana kwamba hatumjali.
Ili nikazie mada yangu, acha nikuulize, je! Wewe unajisikiaje wakati mtu anasahau jina lako? Ni kama inapunguza mara moja wema wao walioweza kuonyesha mwanzoni. Pia inakukwamisha usiweze kuendelea kujenga uhusiano mzuri nao.
Mungu ndiye Muumba wa viumbe vyote. Anajua kila kitu, ana uwezo wote, amejaa upendo. Yuko sehemu zote. Lakini kamwe hajasahau hata jina moja.
Isaya 43:1 Lakini sasa, BWANA aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.
Alimwitaje Yakobo? Nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.
Wewe na mimi hatuko namba fulani kwake Mungu – labda 4,465,970 au 4,465,971, hapana. Hata kama yeye aliumba kila kitu , hata kama ana majukumu mengi – yaani hatuwezi hata kuanza kufikiria majukumu aliyo nayo, ni mengi sana ,si ndiyo?! – pamoja na hayo … anajua jina lako na Hawezi kulisahau. Anakuita kwa jina lako.
Je! Kujua hayo yanakwambia nini leo hii, kuhusu jinsi Mungu wetu wa ajabu anavyokujali na kukupenda?
Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.