Kuzaa Matunda Wakati wa Uzee
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 92:12-15 Mwenye haki atasitawi kama mtende, atakua kama mwerezi wa Lebanoni. Waliopandwa katika nyumba ya BWANA watasitawi katika nyua za Mungu wetu. Watazaa matunda hadi wakati wa uzee, watajaa utomvu, watakuwa na ubichi. Watangaze ya kuwa BWANA ni mwenye adili, Mwamba wangu, ndani yake hamna udhalimu.
Hakuna anayependa kuona kitu kinapotea bure. Haieleweki, sindiyo? Kama bado una kitu ambacho kingekufaa kuzalisha faida na kuletee matunda, kitu ambacho kingesaidia watu wengine, ungekubali kitupwe kama takataka?
Nilishtushwa juzi na habaro moja niliyoisoma kwenye gazeti, ni habari inayomhusu mzee mmoja mwenye umri wa zaidi ya miaka 90. Alizaliwa katika kijiji kidogo kisichojulikana. Jina lake ni Everald Compton na ameishi maisha ya ajabu. Alichangia katika zoezi la kumfungua Nelson Mandela. Amesimia harambee za kukusanya ma-milioni kwa ajili ya mashirika yanayosaidia maskini. Amekuwa tajiri bila kutafuta mali. Yeye ndiye alitetea sana serikali walete reli kwao ili wakulima waweze kusafirisha mizigo yao.
Yaani, ameishi maisha yasiyo ya kawaida. Sasa hivi ni mzee sana. Si muda mwafaka wa kupumzika? La! Bado ana mipango mikubwa: “Kila niamkapo asubuhi,” anasema, “Ninajipongeza kwa kutoka kitandani. Lakini baadaye ninatafakari, Je! Kwa nini bado niko hai hapa duniani?”
Zaburi 92:12-15 Mwenye haki atasitawi kama mtende, atakua kama mwerezi wa Lebanoni. Waliopandwa katika nyumba ya BWANA watasitawi katika nyua za Mungu wetu. Watazaa matunda hadi wakati wa uzee, watajaa utomvu, watakuwa na ubichi. Watangaze ya kuwa BWANA ni mwenye adili, Mwamba wangu, ndani yake hamna udhalimu.
Kinachohuzunisha ni kuona wazee wengine wakistaafu, wanakaa tu wakisubiri siku ya kuzikwa. Ni kupoteza bure vipaji vyao na uzoefu mkubwa walio nao.
Na Mungu hataki vipotee bure. Hata tunapokuwa wazee, bado inatubidi tuendelee kuzaa matunda kama miti mibichi yaani vijana. Bado tuko hapa ili tudhihirishe wema wa Bwana.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.