Kwa Ajili Yetu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
2 Wakorintho 5:21 Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.
Kwenye maisha kuna wakati inabidi umsaidie mtu japo inaweza kukugharimu sana; yaani ni kujitolea. Lazima utaumia.
Nadhani umewahi kufanya hivyo, hata mimi nimewahi kufanya hivyo. Bila shaka itabidi usaidie kwa jinsi hiyo tena kabla ya kumaliza maisha yetu ya hapa chini. Lakini fikiria kidogo, ingekuwaje kama ungechukua mizigo yote ya watu wote wa wa duniani na kuibeba mabegani?
Tunajua ni vigumu kuchukua mizigo ya mtu mmoja; tukichukua ya wawili au watatu wakati mmoja, ni mzigo mzito usiobebeka. Sasa ulimwengu wote,mmh, itawezekana kweli? Lakini ndivyo alivyofanya Yesu kwa ajili yako wewe na mimi pale alipokufa msalabani.
2 Wakorintho 5:21 Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.
Msalabani pale, Yesu alichukua juu yake dhambi za watu wote wanaoishi duniani, waliopo sasa, na hata watakaozaliwa. Si kwamba aliteswa vibaya mno katika mwili wake tu, lakini pia, alikuwa amebeba dhambi za ulimwengu wote katika mwili wake, kama mzigo rohoni na katika hisia zake, ni mzigo usioelezeka.
Kwanini … kwanini sasa alikubali? Ili katika yeye, wewe na mimi tuweze kuwa wenye haki mbele za Mungu. Ili wakati tunaleta maisha yetu pale chini ya msalaba wake, tuweze kusamehewa. Ili, kupitia imani yetu ndani ya Yesu, wewe na mimi tuwekwe huru, tuweze kufanywa kuwa wale Mungu alikusudia tuwe wakati anatuumba. Hii ndiyo habari njema ya Yesu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.