Kwanini Kuhangaikia Utakatifu?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Petro 1:14-16 Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
Kuwa mwema na kutenda mema huwa ni vigumu saana, kwani kuna faida gani ya kuwa mwena na kutenda mema, si kujihangsisha tu!
Jaribu kukumbuka ni lini ulijikuta unaogelea kinyume cha mkondo wa maji – yaani kinyume na utamaduni wa jamii, na mwishowe ukabanwa na rika yako au kinyume cha mgogoro wa familia – ukajaribu kuwa mwema na ukatenda mema, hivi ilikuaje?
Hatimaye ulifikia mahala ukajiuliza, “Ni kwanini nisumbuke hivi?, Niache tu. Acha niende na mkondo wa maji.” Kwasababu kuwa tofauti na wengine ni kazi ngumu.
Kusema ukweli, hii ndio maana ya neno lile, utakatifu – kuwekwa pembeni au kuwekwa wakfu kwa ajili ya kutimiza makusudi ya Mungu. Ina maana, ni kuwa tofauti na watu wa ulimwengu huu, katika upendo, maadili na mwenendo … kwa sababu sisi ni mali yake. Lakini kama ni ngumu hivi, kwanini kuendelea kuhangaika?
1 Petro 1:14-16 Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
Kwanini mtu ahangaike? Kwasababu wakati mtu anapomjua Mungu, huwa anafahamu yaliyo bora. ni lazima umtii Mungu na uwe tofauti na wengine, uwekwe wakfu … kwa sababu inabidi ujue hakika kwamba Mungu amekuteua.
Isitoshe, elewa kwamba ni agizo la moja kwa moja la Mungu kwako: Utakuwa mtakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.