... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Laghai Kuliko Wote Duniani

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 8:44 Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.

Kuna mtu aitwaye Bernie Madoff, aliyewahi kuwa mwenyekiti wa bodi ya soko la hisa iitwayo Nasdaq.  Yeye ndiye aliyeweza kubuni njama ya kutapeli watu wengi kwa hela nyingi kuliko wote katika historia ya binadamu.  Sikiliza kiwango alichoweza kuiba, ni dola za kimarekani biliyoni 64 na nukta 8!

Njama ya namna hiyo ni udanganyifu mpana sana.  Yaani kampuni fulani ya uwekezaji kwenye soko la hisa wanapokea hela za watu wakiwaahidi faida kubwa katika marejesho.  Lakini badala ya kuziweka kwenye soko lile, wanaziiba tu.  Ni kweli wanaweza kutoa malipo ya kawaida ya riba ya kila mwezi kidogo kidogo hata kumrudisha mtu anayedai hela zake zote lakini huku wakitumia hela zingine zilizowekwa hivi karibuni na wateja wapya.  Yaani ni mfumo ambao hauwezi kuendelea muda mrefu, lazima usambalatike kwa sababu hela zile nyingi zilizowekwa mwanzoni tayari zimeishaliwa.

Lakini ingekuwaje kama ningekwambia habari ya utapeli mkubwa zaidi ulioenea kote duniani tangu mwanzo?  Yaani, udanganyifu mkubwa mno uliosababisha hasara kwa watu mamilioni, si kwa kuharibu mali zao tu, hata kuhatarisha uhai wao milele daima.

Siku moja Yesu aliweza kuwaambia watu wasio wazuri maneno yafuatayo:

Yohana 8:44  Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda.  Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake.  Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.

Uongo wake Shetani daima unatwambia kwamba maisha ni mazuri tu.  Ule, unywe na ufurahi.  Hakuna kutoa hesabu kuhusu matendo yako.  Na hata kama kungalikuwepo, wewe si mtu mbaya.

Lakini mfumo wake wa kututapeli siku moja utasambalatika wakati tutasimama mbele zake Muumba wetu.  Usimwamini Ibilisi.  Yeye ni baba ya uongo.  Umwamini Yesu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy