Lengo ni Nini?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Warumi 5:1,2 Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.
Hivi! Mungu alikuwa na makusudi gani kupanga habari hii ambayo kwa sasa tunaiita “Krismasi”? Ni kweli, Krismasi hii tunayeisherehekea leo imebadilika sana. Lakini hata hivi tunaweza kuuliza hivi, Kama Mungu yupo kweli kweli, kwa nini angemtuma Mwanae ulimwenguni kwetu?
Kwetu tunapoishi, ninakiri kwamba ujio wa Yesu duniani umebadilishwa kabisa na kupotosha lengo lenyewe la sherehe . Kwa watu wengi, ni suala la biashara tu, wakiingiza hela nyingi kwa mauzo ya zawadi, nguo na vyakula. Haifanani kabisa na lengo na madhumuni ya Mungu. Wengine pia, hawasherehekei Krismas hata kidogo.
Kwa hiyo, tukisogelea sherehe hii inayofanyika kila mwaka, sherehe ya Kris-masi, tuchunguze kwa pamoja mpango wa Mungu.
Warumi 5:1,2 Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.
Kwa hiyo, kwa yule anayemwamini Yesu, kuna zawadi ya kupokea, zawadi ya ajabu ambayo ingetushinda kuielewa. Licha ya yale yote tuliyoyatenda, sasa tuna msimamo sahihi mbele zake Mungu kupitia Yesu. Tuna amani naye kupitia Yesu. Tunaweza kufurahia baraka za neema yake kupitia Yesu. Tunaweza kufurahia matumaini ya hakika kwamba tutashirikishwa katika utukufu wa Mungu kupitia Yesu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.