... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Lengo ni Nini?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 138:7,8 Nijapokwenda kati ya shida utanihuisha, utanyosha mkono juu ya hasira ya adui zangu, na mkono wako wa kuume utaniokoa. BWANA atanitimilizia mambo yangu; Ee BWANA, fadhili zako ni za milele. Usiziache kazi za mikono yako.

Listen to the radio broadcast of

Lengo ni Nini?


Download audio file

Ni kama kuna aina tatu ya vipindi vya maisha.  Mambo yanaweza kuwa yanaenda shwari kabisa, au – kama unavyojua – yakiwa kawaida tu. Lakini kwa sababu moja au nyingine, maisha yanaweza kutuharibikia.

Haijalishi uko wapi, iwe kwenye vipindi vizuri au vya kawaida au vigumu, hali ya kujisikia umepoteza lengo inaweza kuibuka. Tunauliza, Je!  Lengo ni nini?  Malengo ya maisha yangu ni yapi?  Je!  Mimi kuwepo duniani imeleta mabadiliko gani? 

Kukosa jibu la maswali hayo inaweza kusababisha tukatishwe tamaa, hata kama mambo mengine yanaenda kawaida.  Mfalme Daudi alipitia vipindi hivyo vyote maishani mwake.  Sasa wakati anatafakari hali ya vipindi vigumu, aliweza kutoa dua hii mbele za Mungu: 

Zaburi 138:7,8  Nijapokwenda kati ya shida utanihuisha, utanyosha mkono juu ya hasira ya adui zangu, na mkono wako wa kuume utaniokoa.  BWANA atanitimilizia mambo yangu; Ee BWANA, fadhili zako ni za milele.  Usiziache kazi za mikono yako. 

Ni kama alikuwa amefundishwa kupitia vipindi vigumu na kumtegemea Mungu wakati wa hatari. Alijua kwamba Mungu angenyosha mkono wake na kumuokoa.  Lakini cha msingi ni kwamba … hata kama lengo la Mungu halikuwa dhahiri machoni pa Daudi, lakini Daudi alifahamu kwamba, Bwana atamtimilizia lengo. 

Kila kiumbe kina lengo lake – kila mmea, kila mnyama, na kila mwanadamu– ana lengo lake; lengo alilopewa kabla ya uumbaji.  Hata kama huoni vizuri lengo la maisha yako, kumbuka hili:  Mungu alikuumba akiwa na kusudi maalum na atatimiza lengo lake kwa ajili yako. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.