Maelekezo ya Kufanya Amani (2)
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wakolosai 3:12-14 Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.
Tukisema ukweli bila kuficha, ni kwamba, mtazamo wako dhidi ya watu wanaokusumbua unaweza kulinda amani ya Mungu ndani yako au unaweza kukukosesha amani, huwa inategemeana. Amani yako haitokani na mienendo yao, hapana. Bali inatokana na namna wewe mwenyewe unavyoamua kuwaitikia. Ni kweli kabisa.
Pengine hautafurahi kusikia hilo. Ni rahisi sana kusuta kidole kwa wale wakorofi wanaokukosesha amani; yaani wale wale wanaokusumbua tena na tena na kukuvurugia amani na ustawi.
Ni kweli, wangepaswa kutenda mema. Wasingefanya yanayotukosesha amani… Lakini yameshatendeka!. Huwezi kuyarudisha nyuma.
Jana tuliona hatua ya kwanza katika suluhisho la Mungu kwa matatizo kama hayo. ililenga yale nimeyotoka kusema sasa hivi: kwamba inategemeana na mtazamo wako dhidi yao (na wangu pia).
Wakolosai 3:12,13 Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
Badala ya kukwazika, mtazamo wako wa huruma, utu wema, unyenyekevu, upole na msamaha … hayo yote yanakurejeshea amani.
Lakini kuna kitu kingine kikubwa, kitu ambacho ni muhimu zaidi kinachounganisha yale yote, kitu kinachowezesha maadili.
Wakolosai 3:14 Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.