Maelekezo ya Kufanya Amani (3)
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wakolosai 3:15 Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.
Ni kipi kinasukuma mawazo yako kila siku? Ni yapi yanayosababisha ufanya kile unachokifanya? Ni yapi yanasababisha uwe kama ulivyo? Karibia watu wote, kama ni wa kweli, watajibu kwamba; ni mazingira yao pamoja na watu wanaowazunguka na mahali wanapojikuta. Mara nyingi tunakuwa kama tulivyo kwa sababu ya jinsi tunavyoitikia matukio.
Ebu fikiria kwanza. Ikiwa ulikulia katika nyumba yenye upendo ukiwa na wazazi wazuri hata kama hawakukamilika … lazima uwe mtu tofauti na mwingine aliyekulia kwenye kituo cha mayatima na kuhamishwa-hamishwa makazi bila kuwa na mtu wa kumpenda kabisa.
Ni hivyo hivyo hata kwa watu wazima, yaani mazingira yetu ndiyo yanaongoza mawazo yetu. Mfano, mtu akiwa na ajira ya hakika ni tofauti na mtu aliyekosa kazi; ndoa yenye furaha ni tofauti na watu walioachana; mahusiano mazuri nayo ni tofauti mahusiano yenye migogoro. Hayo yote yana mgongano mkubwa wa kutufanya kuwa kama tulivyo sasa.
Lakini, Ni sahihi kabisa mtu kuruhusu mazingira na matukio na watu wengine walioko huko kuwa na msukumo mkubwa maishani mwake? Au kuna njia mbadala iliyo bora?
Wakolosai 3:15 Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.
Tuwe tayari kukabiliana na maisha kwasababu ni kupanda na kushuka. Yaani kuna furaha na kuna huzuni. Kuna tufani na dhoruba lakini kuna siku zilizo shwari pia. Je! Unapenda kupeperushwa hivyo daima?…jibu ni hapana!
Amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu.
Ukipambana na maisha, uwe na shukrani kila wakati. Kwa sababu ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja.
Kadiri mtu anavyomsogelea Yesu, ndivyo anavyozidi kuwa na amani maishani mwake.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.