... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mafao ya Maonyo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waebrania 12:10,11 Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake. Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.

Listen to the radio broadcast of

Mafao ya Maonyo


Download audio file

Sijaona mtu anayependa maonyo, au mtu anayefurahia kuwekwa chini ya nidhamu na kukaripiwa kwasababu ya mwenendo wake. Sijui kwako wewe?

Watu wengi nikiwemo mimi – wanajidhibiti wenyewe.  Yaani tuna uwezo wa kujiwekea nidhamu katika sekta fulani ya maisha.  Mfano, mimi nimejizoeza kuamka mapema sana alfajiri kila siku na kuchukua muda wa kuwa mbele za Bwana, kisha baadae naandaa vipindi kama hiki.

Lakini hakuna aliyekamilika.  Na mimi nina madhaifu kama vile wewe ulivyo.  Kwahiyo kuna wakati mke wangu ananionya nijirudi.  Pia, katika huduma yetu bodi inaweza kuwa na mawazo tofauti na ya kwangu.  Wanatoa mitazamo yao juu yangu, na kuna wakati wananionya na hata kunirudi yaani kunirekebisha.

Tusisahau pia kwamba … na Mungu anahusika na swala la nidhamu!

Waebrania 12:10,11  Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.  Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.

Na kwa kweli, hakuna anayefurahia adhabu – kutoka kwa binadamu au kwa Mungu.  Lakini mafao ya adhabu  ni makubwa kiasi cha kufanya maumivu kuonekana kama si kitu.  Kuna mfanya biashara mkubwa Mmarekani aitwaye Jim Rohn aliwahi kusema hivi, “Lazima sote tuumie kwa njia moja ama nyingine, aidha aumie chini ya nidhamu; au aumie katika majuto.”  Ni kweli kabisa … Kila adhabu kwa wakati wake huwa inaonekana kama si kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.   

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy