Makadirio ya Thamani
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wafilipi 3:20 Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo.
Mtu tunayemruhusu kutushawishi katika fikra zetu hata katika matendo yetu pamoja na vishawishi vingine, ni habari tusiyoifikiria sana. Katika zama hizi zinazosukumwa na njia za mawasiliano, tumezoea kumeza “vikorokoro” vyote bila hata kufikiria. Lakini kuzembea hivyo ni hatari kabisa.
Ushawishi – ni kitu chenye nguvu. Kama tulivyoangalia siku hizi chache, kukubali kushawishika na watu wema ni baraka kubwa. Yaani, wacha Mungu wanaokuwa vielelezo vya kuigwa, ni kama alama za barabarani zilizowekwa kutuelekeza njia sahihi.
Lakini tukiruhusu tushawishike na watu wabaya hatimaye tutaathirika. Tukishawishika na watu binafsi, matangazo ya biashara, mitindo ya kisasa katika jamii, vyama ya siasa, mifumo ya imani inayoshindana … yaani kushawishika na wale ambao Mtume Paulo anawaita “adui wa msalaba”, ni lazima itatuletea madhara.
Sasa mtu atawezaje kupambanua kati ya mema na mabaya, washawishi wacha Mungu na washawishi waovu? Siyo vigumu. Mtu angetumia mfumo wa kukadiria kilicho na thamani kuliko vyote:
Wafilipi 3:20 Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo.
Wewe na mimi, si wenyeji wa ulimwengu huu. Kama vile Yesu alivyosema, sisi kama yeye tumo duniani, bali si wa dunia hii. Kwahiyo, kama unatatanishwa na upambanuzi huo, mtazame Yesu, anayeleta mfumo wa kukadiria kilicho na thamani zaidi, kupima kila kitu kwa kanuni ya mbinguni.
Watu, makampuni, makabila … waache waseme, lakini sisi kama tunamuita Yesu kuwa Bwana wa maisha yetu, yeye ndiye kanuni yetu; Yeye ndiye mtawala tunayemtumia kwa kuwapima hawa wanaotaka kutushawishi.
Na kama wanaonekana na upungufu, basi achana nao kabisa. Labda utaumia kwanza, lakini kumbuka kwamba unamtazamia Yesu Mwokozi wako arudi. Hii ndiyo ya muhimu kuliko vyote.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.