... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mambo Ambayo Bwana Alikuandalia

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 2:8,9 Ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu; lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.

Listen to the radio broadcast of

Mambo Ambayo Bwana Alikuandalia


Download audio file

Wakati unajaribu kuishi vizuri na kuwa mtu mwema mwadilifu, lakini wote ambao wanaokuzunguka wanatenda visivyo – unaweza kuanza kujiuliza, “Je!  Kwa nini kujisumbua hivi, kuna faida gani?”  Ni swali nyeti, Je!  Kuna faida gani katika kutenda mema?

Dietrich Bonhoeffer alikuwa mchungaji Mjerumani akawa pia mwanathiolojia na anajulikana kuwa mmoja wao walioupinga udikteta wa Hitler na maovu yake – maangamizi aliyokuwa anayoyaongoza.  Bonhoeffer yeye alisimama kidete na kupaza sauti kwa kusema, “Hapana, haiwezekani!”

Sasa matokeo ya upinzani wake wa hadhara, ni kwamba alikamatwa na upelelezi uitwao Gestapo na kufungwa miaka miwili katika kambi ya wafungwa wa siasa.  Baadaye alishitakiwa kushiriki njama ya kumwua Hitler na hatimaye alinyongwa tarehe 9 Aprili 1945, wakati utawala wa Nazi ulikuwa unaporomoka.  Kwa hiyo, swali linakuja, je!  Msimamo wake ulikuwa na faida gani?

Hili ndilo swali Mtume Paulo alilozua wakati aliliandikia kanisa la Korintho zamani kwenye karne ya kwanza wakati kanisa lile lilikuwa linavutwa huku na huku kati ya wema na uovu.

1 Wakorintho 2:8,9  Ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu; lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.

Miaka elfu mbili kabla ya Bonhoeffer, Yesu pia alisimama kidete na kukemea uovu kwa ujasiri, msimamo uliomgharimu uhai wake.  Lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. 

Vuta subira.  Faida inakuja kabisa.

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy