Mantiki ya Upendo
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Warumi 5:9 Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.
Kuna neno ambalo lilinisumbua miaka mingi. Inawezekana, tukielekeza mawazo yetu kwenye Krismasi, kwamba hata wewe umesumbuliwa nalo. Ni hili: Kwa nini Mungu alimtuma Yesu duniani, afanyike mwanadamu na hatimaye kufa msalabani, ikisemekana kwamba alikufa kwa ajili ya dhambi zetu ili tupate kusamehewa? Kwa nini hakutusamehe bure tu? Singelikuwa rahisi zaidi?
Unajua? Miaka ile ya kwanza baada ya mimi kuweka imani yangu ndani ya Yesu, baada ya kuwa mmoja wa wanaoitwa “Wakristo”, nilikuwa bado sijawa na jibu la swali lile: Kwa nini Mungu asingetusamehe bure tu, bila kumtuma Yesu aende msalabani; bila kutwambia kwamba inatubidi kumwamini ili tuweze kuokolewa na dhambi zetu?
Ninakwambia kwamba bila jibu la swali hilo, habari hii yote ya Krismas haieleweki hata kidogo. Nilihitaji kuelewa – sote tunahitaji kuelewa mantiki iliyoendesha zoezi hili kubwa la upendo – yaani kusulibiwa kwa Yesu kwa ajili ya dhambi zetu.
Warumi 5:9 Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.
Tuokolewe na ghadhabu ya Mungu. Na suala la ghadhabu linasisitizwa hata na mahakama yetu iliyoandaliwa na wanadamu walioumbwa kwa mfano wa Mungu.
Tendo lo lote lisilo la haki lazima liadhibiwe. Ndivyo ilivyo, hakuna kukwepa. Sasa matendo yetu yote ya kumwasi Mungu lazima yawe chini ya ghadhabu yake, hii ndiyo haki. Lazima yaadhibiwe, tuhukumiwe.
Lakini kutokana na pendo lake kuu, ghadhabu yake ilimwangukia Mwanae kupitia dhabihu ya damu iliyotolewa pale msalabani. Ili … tuokolewe na ghadhabu kwa yeye.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.