Martha au Mariamu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Luka 10:38-42 Ikawa katika kuenenda kwao aliingia katika kijiji kimoja; mwanamke mmoja jina lake Martha akamkaribisha nyumbani kwake. Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake. Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie. Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi; lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.
Mara nyingi huwa nina kazi za ziada, nikiwa bize sana kwa kutimiza wajibu wangu huwa inaniwia vigumu kutenga muda mzuri kukaa na Yesu kwa sababu ya uchovu mwingi. Je! Wewe umewahi kujikuta katika hali kama hiyo?
Nafahamu kwamba si kila mtu yuko bize kila wakati. Hata mimi huwa ninatenga muda wa kupumzika kila siku na kila wiki. Lakini hata hivyo nafikiri ulielewa maneno yangu ya utangulizi, si kweli?
Maisha, familia, ajira, na kujipanga vizuri katika ulimwengu wetu huu changamani wenye mitandao, jamani swala la kumtumikia Yesu sio rahisi kwa sababu ya majukumu mengi tuliyo nayo. Lakini tusifikiri kwamba kitendawili hicho ni cha karne yetu ya 21 tu.
Luka 10:38-42 Ikawa katika kuenenda kwao aliingia katika kijiji kimoja; mwanamke mmoja jina lake Martha akamkaribisha nyumbani kwake. Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake. Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie. Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi; lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.
Au kama vile Charles Spurgeon alivyowahi kusema: “Kuna wakati nilikimbizana na Martha kutimiza yale Kristo aliyohitaji nimfanyie, lakini nadhani inanibidi nizidi kukaa na Mariamu ili nipokee yale ninayohitaji kutoka kwa Kristo Yesu.”
Tenga muda wa kukaa na Yesu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.