... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mashabiki Kigeugeu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 2:23-25 Hata alipokuwapo Yerusalemu kwenye sikukuu wakati wa Pasaka, watu wengi waliamini jina lake, walipoziona ishara zake alizozifanya. Lakini Yesu hakujiaminisha kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote; na kwa sababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu; kwa maana yeye mwenyewe alijua yaliyomo ndani ya mwanadamu.

Listen to the radio broadcast of

Mashabiki Kigeugeu


Download audio file

Kwa kuwa tumeumbwa tuishi kijamii, tunafurahi pale mahusiano yetu yanapokuwa shwari.  Kukaa kijamii inatakiwa uwapendeze wengine na wao pia wakupendeze. Lakini katika swala la kujaribu kupendeza watu wengine, mtu anaweza kupita kiasi.

Nafikiri unajua inavyokuwa, kwenye uhusiano wowote kuna kutoa na kupokea, hapo ndo kuna kuwa na uwiano mzuri, sasa watu wanapofaulu kupata uwiano ule, hapo mahusiano huwa yanapendeza sana, si ndiyo!? 

Lakini; kidogo kidogo, matazamio ya watu wengine yanaweza kutawala maisha yetu. Kila mtu anapenda kupendwa, kwa hiyo, bila kufahamu, mtu anaweza kuanza kucheza kwa pigo la ngoma ya watu wengine huku akiongozwa kama vile katuni, tena isitoshe, anaongozwa na watu ambao mara nyingi si wenye maadili.  Yesu alifahamu hayo vizuri sana. 

Yohana 2:23-25  Hata alipokuwapo Yerusalemu kwenye sikukuu wakati wa Pasaka, watu wengi waliamini jina lake, walipoziona ishara zake alizozifanya.  Lakini Yesu hakujiaminisha kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote; na kwa sababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu; kwa maana yeye mwenyewe alijua yaliyomo ndani ya mwanadamu. 

Tena Yesu alifanya vizuri kutokujiaminisha kwao, kwasababu,  baada ya miaka michache, watu walewale walishawishika kiasi cha  kupiga kelele kwa jazba, wakisema, “Msulubishe!  Msulubishe!” 

Sasa angalia.  Haijalishi wewe ni mzuri kiasi gani, kusema ukweli, wale watu ni vigeugeu.  Watu wa namna hiyo hawawezi kushindwa kukuhukumu kulingana na hisia za matamanio yao. 

Ndiyo, inapendeza kupongezwa pale unapotenda vizuri.  Lakini kama vile Yesu, alivyojaribu kupambanua mioyo yao.  Na wewe jaribu kupima kama makasudi yao ni meupe au la. Usiishi kwa kujaribu kupendeza umati wa watu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy