... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Maswala ya Familia

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yoshua 23:15 Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA.

Listen to the radio broadcast of

Maswala ya Familia


Download audio file

Itafikia wakati kila mmoja wetu atapaswa kuamua mwenyewe kama atamwamini Yesu na kumtumikia kama Bwana wake au kumkataa na kufuata njia yake mwenyewe. Hakuna njia ya katikati.

Natumaini kwamba umeshafanya maamuzi ya kumfuata Yesu kama vile nilivyofanya mimi. Pia, ni maamuzi mtu anayopaswa kuyafanya daima … kila siku za maisha yake hapa duniani kwa kila wazo, kwa kila tendo. 

Lakini wengi wana tabia ya kufikiri na kuamua kama mtu binafsi si kama mmoja wa familia fulani.  Ndio, bado kuna utamaduni unaothamini familia sana, Lakini kadiri watu wanavyozidi kupata mali ndivyo wanavyozidi kutokujali tena ndugu na jamaa. 

Ndio maana Andiko lifuatalo linakuja kwa muda mwafaka. Haijalishi unaishi wapi au una tamaduni gani, bado linakulenga: 

Yoshua 23:15  Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA. 

Kumbe, uamuzi wa kumpenda Mungu, kumuamini Yesu na kumwishia maisha yote inahusu familia zetu, si kwa ajili ya mtu binafsi tu.

Mungu anathamini familia yako sana sana.  Kwa hiyo, niulize, je! Wewe na familia yako, mtamtumikia nani?  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.