Matendo Makuu ya Mungu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yeremia 32:17 Aa! Bwana MUNGU, tazama, wewe umeziumba mbingu na nchi, kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyoshwa; hapana neno lililo gumu usiloliweza.
Je! Umewahi kuwa na shauku ya kutenda jambo “kuu” kwa ajili ya Mungu? Je! Umewahi kuota ndoto kwamba ametenda makuu maishani mwa watu wengine kupitia wewe? Lakini kwa watu wengi, hua inabaki kuwa ndoto tu.
Mtu awaye wote anayempenda Yesu, lazima amewahi kuwa na ndoto hizo; yaani dhana kwamba tungeweza kutenda jambo la ajabu kwa ajili yake; jambo ambalo lingeweza kutikisa ulimwengu na maisha ya wanaotuzunguka. Lakini mara nyingi tu, hali halisi ya maisha ya kila siku na shughuli zake zinatubana tusiweze kutimiza makusudi yetu.
Basi! Yatosha ile swala la ndoto! Kwa hiyo tunarudi kwenye hali ya kawaida. Shida iliyopo ni kwamba tunafuatilia zile ndoto kwa mtazamo usio sahihi. Tunaziangalia kwa kufikiria uwezo wetu jinsi ulivyo badala ya kuchunguza yale ambayo Mungu tayari ameshaanza kufanya.
Nabii Yeremia aliwahi kuandika hivi katika Agano la Kale:
Yeremia 32:17 Aa! Bwana MUNGU, tazama, wewe umeziumba mbingu na nchi, kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyoshwa; hapana neno lililo gumu usiloliweza.
Kipindi taifa la Israeli walikuwa wanakumbana na matatizo mengi, Mungu aliwakumbusha ni nani aliye na uwezo mwingi. Yule ambaye kwake, hakuna neno lisilowezekana.
Kwa mtazamo wetu, mambo makuu daima yanaonekana kuwa yasiyowezekana.
Kulikuwa mishonari wa karne ya 19 huko China aitwaye Hudson Taylor aliyekumbana na upinzani mwingi mkali. Lakini baada ya kumtumikia Mungu miaka mingi, aliweza kuandika hivi: “Nimegundua kwamba kuna hatua tatu katika kila tendo kuu la Mungu … kwanza haliwezikani, pili linakuwa gumu, tatu linakuwa limetendeka tayari.”
Matendo yale makuu tunayoota yatendeke, si matendo yetu, bali ni matendo ya Mungu … ambayo kwake, hakuna neno lisilowezekana.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.