Matumaini Yaliyo Safi
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Yohana 3:3 Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.
“Usafi” ni neno ambalo tunalipenda. Mfano, dhahabu safi, furaha tupu isiyoghoshiwa … lakini je! Umewahi kukutana na mtu aliye safi kabisa? Yaana mtu aliye mwadilifu katika fikra zake akiwa na makusudi yaliyo safi kabisa, pia akitenda na kuongea kufuatana na uadilifu wake? Watu kama hao wanapatikana kwa nadra sana.
Ukifikiria habari ya filamu na vipindi kwenye TV ambavyo unavyopenda zaidi, bila shaka utataja habari ya shujaa fulani anayepambana na maisha licha ya mazingira magumu, akiishi maisha ya wema na fadhili, upendo na hatimaye anaonekana kuwa mshindi mkubwa.
Hiyo ndiyo dhana ya usafi au utakatifu. Ni wema unaopambana na vipingamizi vingi. Ila, katika maisha yetu ya kila siku, tunachafuliwa na ulimwengu huu. Tunataka kuwa “wasafi” yaani “watakatifu”, lakini maisha yanachanganya sana. Kuna wakati inatubidi kuchagua yasiyo mabaya zaidi katika maisha, yaani hakuna chagua lililo jema.
Sasa katika mazingira machafu kama hayo, bado Mungu anayo yakutwambia:
1 Yohana 3:3 Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye [yaani Mungu mwenyewe] alivyo mtakatifu.
Mimi naona kwamba inatubidi mara kwa mara kukumbushwa kwamba kuna faida kubwa kujitenga na uchafu watu wa dunia wanatupiana, ni vema kujitakasa na kuwa safi katika mawazo, maneno na matendo.
Na hii ni kwa sababu Mungu yeye ni mtakatifu. Sasa, kama tumeweka matumaini yetu kwa Mwanae Yesu, yule aliyetukomboa kutoka utumwa wa dhambi kwa kulipa pale msalabani gharama iliyotisha tuliodaiwa, basi inabidi na sisi tuwe watakatifu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.